Kamati ya Bunge yatoa makucha yake

Friday March 22 2013

By Fidelis Butahe, Mwananchi

Ruvu. Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) jana iliibana Menejimenti na Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Ranchi za Taifa  (Narco), ikiitaka kutoa maelezo ya kina sababu za  kusimama kwa mradi wa ujenzi wa machinjio ya kisasa yaliyokuwa yajengwe  eneo la Ruvu mkoani Pwani.

Akizungumza mara baada ya kutembelea eneo hilo jana, Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Deo Filikunjombe alisema kwa muda mrefu mradi umesimama kutokana na ukosefu wa fedha.

Tanzania iliwahi kuwa na eneo la machinjio ya kisasa ya Tanganyika Packers  jijini Dar es Salaam, lakini lilifungwa mwaka 1978, mwaka 2007 Serikali ilihimiza ujenzi wa machinjio na viwanda vya kusindika nyama, hivyo kuanza kwa jitihada za kujenga machinjio hiyo.

Advertisement