Papa, maaskofu kujadili unyanyasaji wa kingono

Rome,Italia. Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis anatarajia kukutana na viongozi wa kanisa hilo kutoka ulimwenguni katika mkutano wa kilele utakaojadili jinsi ya kukabiliana na unyanyasaji wa kingono unaofanywa na mapadri.

Hii inafuatiwa na madai ya baadhi ya mapadri kuwanyanyasa watawa kwa kuwatumikisha kingono katika makazi ya watawa nchini Ufaransa.

Papa Francis aliamua kuitisha mkutano wa kimataifa baada ya kujadiliana na makadinali tisa ambao aliwateua baada ya yeye kuchaguliwa.

Simulizi za unyanyasaji zimekuwa zikijitokeza katika kila kona ulimwenguni.Na kanisa limekuwa likishutumiwa kwa kutetea uhalifu wa mapadri.

Mkutano huu ambao utahudhuriwa na maskofu wakuu katika kila nchi kutoka katika nchi zaidi ya 130, ndio mwanzo mzuri ambao unaashiria kuwa ugonjwa ambao umekuwa ukilisumbua Kanisa hilo tangu 1980 sumu yake inaweza kutolewa.

Majimbo sita kati ya nane ya Kanisa Katoliki katika mji wa Pennsylvania yalifanyiwa uchunguzi mwaka jana. Mashaidi kadhaa walitoa ushuhuda wao na viongozi wengine wa dini walikubali makosa yao.

“Zaidi ya waathirika 1000 waliobanika walikuwa ni watoto , na shutuma zilikuwa zinawakabili mapadri zaidi ya 300”.

Ripoti yenye kurasa zaidi ya 1,000 ziliangazia unyanyasaji uliofanyika miaka 70 iiyopita. Katika jimbo la Scranton, padri alimbaka msichana na baada ya kubainika ana ujauzito akamwambia atoe.

Katika jimbo lingine, padri alimtembelea mtoto wa miaka saba hospitalini na kumbaka.

Tukio lingine lilikuwa la unyanyasaji kwa mtoto wa miaka tisa la kumwagia maji ya baraka.

Padri Franco Mulakkal aliondolewa katika kanisa moja dogo Kusini Magharibi mwa nchini India na kupelekwa kuwa askofu katika eneo la kaskazini mwa nchi hiyo.