Shule 10 bora matokeo kidato cha sita hizi hapa

Katibu mtendaji wa Baraza la Taifa la mitani (NACTE)  Charles Enock Msonde ikifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari mjini Ungu leo wakati alipokua akitoa taarifa ya matukio ya mtihani wa kidato cha sita kwa mwaka 2019. Picha na Muhammed Khamis

Muktasari:

  • Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya kidato sita mwaka 2018 na kutaja shule kumi bora  zilizofanya vizuri katika mtihani huo

Unguja. Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya kidato sita mwaka 2018 na kutaja shule kumi bora  zilizofanya vizuri katika mtihani huo.

Akizungumza leo Alhamisi Julai 11, 2019 visiwani Zanzibar wakati akitangaza matokeo hayo katibu mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Charles Msonde amesema shule iliyoshika nafasi ya kwanza ni Kisimiri ya mkoani Arusha iliyokuwa na watahiniwa 60.

Msonde amesema Feza Boys ya jijini Dar es Salaam yenye watahiniwa 87 imeshika nafasi ya pili ikifuatiwa na Ahmes ya mkoani Pwani iliyokuwa na watahiniwa 112.

“Mwandet yenye watahiniwa 77 ya mkoani Arusha imeshika nafasi ya nne huku Tabora Boys ya mkoani Tabora yenye watahiniwa 109 imeshika nafasi ya tano,” amesema Msonde.

Kibaha ya mkoani Pwani yenye watahiniwa 172 imeshika nafasi ya sita na kufuatiwa na Feza Girls (watahiniwa 66), St Mary’s Mazinde Juu (216), Canossa (83) na Kemebos (33).