Kilimo kinaharibu zaidi mazingira kuliko ukataji miti kwa ajili ya mkaa

Mkurugenzi Mtendaji wa TFCC, Charles Meshak ( wa pili kulia) akitoa mada katika mjadala wa Jukwaa la Frika linalojadili matumizi ya mkaa, uchumi na mazingira yetu, jijini Dar es Salaam leo. Picha na Edwin Mjwahuzi

Muktasari:

Wakati wadau wakichambua madhara ya mkaa kwa mazingira, Ofisa Misitu Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Charles Meshack amesema Kilimo ndiyo kinaongoza kwa kuharibu misitu kwa asilimia 80


Dar es Salaam. Wakati wadau wakichambua madhara ya mkaa kwa mazingira, Ofisa Misitu Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Charles Meshack amesema Kilimo ndiyo kinaongoza kwa kuharibu misitu kwa asilimia 80.

Akizungumza leo katika mdahalo wa Jukwaa la Fikra jijini Dar es Salaam, Meshack amesema mkaa unaharibu misitu kwa asilimia 13 tu.

"Tusijidanganye kuwa mkaa unaharibu misitu. Kilimo kinaharibu misitu kwa asilimia 80, mkaa ni asilikia 13 tu," amesema Meshack.

Ameshauri kurasimishwa kwa sekta ya mkaa kwa kuwa na chombo maalumu cha udhibiti.

"Lazima turasimishe mkaa na misitu kama ilivyo Ewura (Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji)  kuwe na taasisi huru itakayodhibiti mkaa," amesema.

"Usimamizi shirikishi wa misitu njooni Kilosa, Mvomero mwone watu wanavyotumia mkaa endelevu,” amesema