SIKU YA WANAWAKE DUNIANI: Benki ya NBC yawakumbuka wateja wake

Tuesday March 12 2019

Mkuu wa Kitengo cha Wateja Maalumu wa Benki ya

Mkuu wa Kitengo cha Wateja Maalumu wa Benki ya NBC, Ashura Waziri (kulia), na ofisa katika  kitengo hicho, Nuru Lema (kulia), wakikabidhi maua kwa mmoja wa wateja wao Manka Teweli, dukani kwake jijini Dar es Salaam ikiwa ni moja ya matukio katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani. mcl digital

Peter Edson, Mwananchi

 Dar es Salaam. Katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani Benki ya NBC imesherehekea tofauti siku hiyo kwa kuwatembelea wateja wake mahali walipo ikiwa ni majumbani, maofisini, ama kwenye biashara zao lengo likiwa ni kupokea maoni kutoka kwa wateja hao kuhusu huduma wanazopewa na benki hiyo kulingana na mahitaji yao ya kifedha  

Akielezea kuhusu hatua hiyo Mkuu wa Kitengo cha Wateja Maalumu wa Benki ya NBC, Ashura Waziri amesema wameamua kuwatembelea wanawake kwenye shughuki zao na majumbani ili kuonyesha thamani yao kwao kwani mara nyingi wanawake hao hufika katika matawi ya benki hiyo ila wao hawajawahi watembelea

“leo ni siku ya wanawake duniani, kama wanawake wa benki ya NBC, tumeona tutoke tuje kuwatembelea wateja wetu mtaani ili tuweze kuwafahamu zaidi na kujua changamoto wanazozipa katika biashara zao”, alisema Waziri.

Amesema Maadhimisho ya Siku ya Wanawake, hutoa fursa kwa wadau, na wanawake wenyewe kupima utekelezaji wa maazimio, matamko na mikataba ya Kimataifa, Kikanda na Kitaifa inayohusu masuala ya maendeleo ya wanawake na usawa wa jinsia.

Siku ya wanawake Duniani husisitiza kujenga mshikamano wa wanawake wote duniani, kuhamasisha jamii kutafakari kaulimbiu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake ya kila mwaka; kuelimisha jamii kuhusu jitihada mbalimbali zilizofanywa na Serikali na asasi mbalimbali yakiwemo Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika kuwaendeleza wanawake; na kuhamasisha jamii kuhusu utekelezaji wa sera na mipango mbalimbali ya Serikali yenye lengo la kudumisha Amani, Usawa na Maendeleo.

Kaulimbiu ya Kitaifa ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani kwa mwaka 2019 inasema: “Badili Fikra Kufikia Usawa wa Kijinsia kwa Maendeleo Endelevu”.

Miongoni mwa wateja wa benki ya NBC waliotembelewa katika maadhimisho hayo ni pamoja na Manka Teweli, dukani kwake,  Nkaleni Moria Warioba,  ofisini kwake , Scolastika Ponera, nyumbani kwake na Doreen Nandha, dukani kwake wote wakiwa ni kutoka jijini Dar es Salaam 

Advertisement