Utaratibu wa vijana kujitolea kutoka nje ya nchi waanzishiwa programu

Wednesday April 24 2019

By Nazael Mkiramweni, Mwananchi [email protected]

Dodoma. Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali inatarajia kuweka mkakati wa pamoja wa kuanzisha  programu ya mabadilishano ya shughuli za kujitolea zitakazobainisha utaratibu wa kupokea vijana wa kujitolea kutoka nje ya nchi.

Hayo yamesemwa  leo Jumatano Aprili 24, 2019  na Mkurugenzi Msaidizi Uratibu wa Uwezeshaji Vijana Kiuchumi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Esther Riwa, akifungua mkutano wa Raleigh Tanzania unaolenga kuelezea mafanikio ya shirika hilo kwa vijana.

Amesema kupitia utaratibu huo wa kuanzisha programu ya kujitolea utawezesha kuwafikia vijana wengi zaidi kupata ujuzi, kubadilishana maarifa ili kuleta mabadiliko ya kiuchumi kwa jamii na Taifa kwa ujumla.

Naye ofisa wa mradi wa uwajibikaji wa jamii kupitia vijana,  Peter Lazaro, amesema lengo la mradi huo ni kutoa elimu kwa vijana ili wawajibike.

Advertisement