Binti amkataa baba mzazi aliyemzalisha

Friday April 26 2019

 

By Twalad Salum, Mwananchi [email protected]

Misungwi. Shahidi wa kwanza katika kesi ya ubakaji inayomkabili Jacob Shabani (30) amemkataa baba yake huyo anayeshtakiwa kwa kufanya mapenzi na mwanaye na kumzalisha watoto wawili.

Tukio hilo lilitokea mwaka 2015 kijiji cha Wanzamiso wilayani Misungwi, mkoani Mwanza.

Akitoa ushahidi katika Mahakama ya Wilaya ya Misungwi, shahidi huyo (16) akiongozwa na mwendesha mashatka wa polisi, Ramsoney Salehe, alieleza mkuwa akiwa na miaka 12 mwaka 2015 katika kijiji cha Ng’walogwabagole baada ya mama yake mzazi, Hoja Clement, kufariki dunia alianza kujihusisha kimapenzi na baba yake huku akimtishia kumuua.

“Simtaki baba yangu na sitaki hata kumtazama kwani sijisikii vizuri kitendo alichonifanyia kunilazimisha mapenzi toka mwaka 2015 hadi 2018 alipokamatwa,” alidai shahidi huyo.

Aliendelea kuwa baba yake alimpa ujauzito mara tatu, mtoto wa kwanza alifariki mwaka 2018, mimba ya pili ilitoka baada ya kupigwa alipoenda kwa shangazi yake na mimba ya tatu ni ya mtoto aliyenae.

Hakimu mkazi mfawidhi wa wilayani hiyo, Erick Marley alimpa nafasi mshtakiwa kumuuliza maswali binti yake, akadai kuwa hana maswali kwa kuwa haitambui hiyo kesi.

Marley aliahilisha kesi hiyo hadi Mei 7 huku akiagiza upande wa mashtaka kuleta ushahidi wa watu wanane, mshtakiwa alirudisha rumande baada ya kukosa kumdhamini.

Akisoma hati ya mshtakiwa kesi namba 2 ya mwaka 2018, mwendesha mashataka wa polisi, Salehe alisema mshitakiwa anakabiliwa na kosa la kufanya mapenzi na mwanae.

Alisema mshitakiwa huyo alitenda makosa hayo mwaka 2015b hadi 2018 katika kijiji cha Mwalogwagole na Wanzamiso na binti yake mwenye umri wa miaka 12 ambapo pia alimpatia ujauzito mara tatu.

Advertisement