Kipindi cha televisheni cha udaku chafutwa baada ya mgeni kufariki saa chache baada ya kuhojiwa

Jeremy Kyle

Muktasari:

Kipindi cha televisheni cha udaku cha nchini Uingereza, Jeremy Kyle Show kimefutwa ikiwa ni miaka 14 tangu kuanzishwa kwake baada ya mgeni kufariki saa chache baada ya kuhojiwa.

Kipindi cha televisheni cha udaku cha nchini Uingereza, Jeremy Kyle Show kimefutwa ikiwa ni miaka 14 tangu kuanzishwa kwake baada ya mgeni kufariki siku chache baada ya kuhojiwa.

Inadaiwa mtu huyo Steve Dymond alifariki dunia siku chache baada ya kushiriki kipindi hicho.

Kipindi hicho huwaumbua wapenzi wasaliti au waliosalitiwa pamoja na kuwakutanisha wapenzi waliohitilafiana ili kusutana.

Taarifa ya ITV inayosimamia utengenezaji wa kipindi, imeeleza kuwa itaendelea kufanya kazi na mtangazaji wake Jeremy katika vipindi vingine.

Ilisema inasikitishwa na kifo cha Dymond na ili kumuenzi imeamua kukiondoa kabisa kipindi hicho.

Hata hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa ITV, Carolyn McCall aliiambia CNN kuwa wamechukua uamuzi huo kutokana na kilichotokea na kuwaomba radhi mashabiki wake waliokuwa wakikifuatilia kwa kuwa watakikosa hewani.