Magufuli atumia simu ya mkononi kuwapiga picha Kikwete, Rais Ramaphosa

Saturday May 25 2019

 

By Muyonga Jumanne, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Nchini Afrika Kusini leo Jumamosi Mei 25, 2019 ni siku ya kukumbukwa kutokana na Rais Cyril Ramaphosa kuapishwa kuwa kiongozi wa Taifa hilo kwa muhula wa pili.

Katika hafla ya kuapishwa kwake iliyohudhuriwa na viongozi wa nchini mbalimbali, akiwemo Rais John Magufuli na Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kiwete kuliibuka matukio mengi ya kufurahisha.

Moja kati ya matukio hayo ni kitendo cha Rais Magufuli kutumia simu ya mkononi kuwapiga picha Rais Ramaphosa na Kikwete.

Tukio hilo limevuta hisia za watu wengi katika mitandao ya kijamii na kushangazwa na Rais Magufuli jinsi alivyoshikilia vyema simu hiyo na kuwapiga picha wawili hao.

Viongozi hao walionekana kufurahia tukio hilo wakiwemo baadhi ya marais wa mataifa mengine waliokuwa pembeni yao.

Rais  Magufuli ameambatana na Kikwete pamoja na makamu mwenyekiti wa CCM, Philip Mangula nchini Afrika Kusini kuhudhuria sherehe hizo.

Ramaphosa ameapishwa na Jaji Mkuu wa Afrika Kusini, Mogoeng Mogoeng.

Hafla hiyo ilipambwa kwa maonyesho ya ndege za kijeshi zilizorushwa angani na askari waliotua kwa miavuli na kupigwa mizinga ya heshima kwa Amiri Jeshi Mkuu huyo.

 

Advertisement