LIVE: BAJETI YA SERIKALI 2019/2020, IKISOMWA BUNGENI JIJINI DODOMA

Dodoma. Watanzania wanatega sikio kumsikiliza Waziri  wa Fedha na Mpango, Dk Philip Mpango akiwasilisha bungeni jijini Dodoma bajeti kuu ya Serikali mwaka 2019/2020.

Leo saa 9: 47 alasiri waziri huyo akiwa amevalia suti nyeusi,  shati jeupe na tai yenye rangi ya bendera aliingia bungeni akiwa na begi lenye bajeti hiyo ya nne tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani.

Wakati akiingia bungeni, Dk Mpango alikuwa na msaidizi mmoja huku baadhi ya wabunge wakifuatilia tukio hilo.

Katika bajeti hiyo ya Sh33 trilioni, Serikali imetenga Sh12.2 trilioni kwa ajili ya kugharamia Mpango wa Maendeleo wa Taifa mwaka 2019/2020.

Kati ya fedha hizo Sh9.7 trilioni ni fedha za ndani na Sh2.5 trilioni ni fedha za nje. Fedha hizo za maendeleo ni sawa na asilimia 37 ya bajeti yote ya mwaka 2019/2020.