Uongozi shule ya kwanza kitaifa matokeo kidato cha sita watoa neno

Shule ya Sekondari ya Kisimiri

Muktasari:

  • Uongozi wa Shule ya Sekondari ya Kisimiri iliyoshika nafasi ya kwanza kitaifa katika matokeo ya kidato cha sita mwaka 2018, umeeleza siri ya mafanikio

Arusha. Uongozi wa Shule ya Sekondari ya Kisimiri iliyoshika nafasi ya kwanza kitaifa katika matokeo ya kidato cha sita mwaka 2018, umeeleza siri ya mafanikio.

Katika matokeo hayo yaliyotangazwa leo Alhamisi Julai 11, 2019 kisiwani Zanzibar na katibu mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Charles Msonde, amesema shule hiyo yenye watahiniwa 60 wa kidato cha sita, imekuwa kinara kati ya 10 zilizofanya vizuri kitaifa.

Shule nyingine ni Feza Boys, Ahmes, Mwandet, Tabora Boys, Kibaha, Feza Girls, St Mary’s Mazinde Juu, Canossa na Kemebos.

Akizungumza na Mwananchi leo mkuu wa shule hiyo,

Valentine Tarimo ametaja mambo yaliyoifanya shule hiyo kuibuka kinara kuwa ni mipango imara, utekelezaji na usimamizi.