Mbunge Mwakajoka wa Chadema akamatwa na polisi kwa tuhuma za mwaka 2018

Thursday July 11 2019Mbunge wa Tunduma (Chadema), Frank Mwakajoka

Mbunge wa Tunduma (Chadema), Frank Mwakajoka 

By Stephano Simbeye, Mwananchi [email protected]

Tunduma. Mbunge wa Tunduma (Chadema), Frank Mwakajoka amekamatwa na polisi ikielezwa kuwa atafikishwa mahakamani muda wowote kujibu tuhuma za kumpiga mtu mwaka 2018.

Akizungumza na Mwananchi leo Alhamisi Julai 11, 2019 kamanda wa polisi Mkoa wa Songwe, George Kyando amesema mbunge huyo amekamatwa leo na atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo.

Amebainisha kuwa Mwakajoka anadaiwa kumpiga mwananchi ambaye hajamtaja jina, kwamba kesi hiyo ni ya muda mrefu

"Kuhusu jina la mtu aliyepigwa hapa sina labda unipe muda ili nilitafute,” amesema kamanda huyo.

Katibu wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) Mkoa wa Songwe, Ayub Sikagonamo amedai Mwakajoka amekamatwa kwa madai ya kumpiga ofisa mtendaji wa mtaa, Deus Mwampashe.

Mbunge huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo.

Advertisement

Advertisement