Uandikishaji wapiga kura waiva Arumeru Magharibi

Muktasari:

Shughuli ya uboreshwaji wa daftari la kudumu la wapiga katika halmashauri ya wilaya ya Arusha litaanza Julai 18 na kukamilika Julai 24, 2019.

Arusha. Shughuli ya kuandikishwa wapiga kura katika  halmashauri ya wilaya ya Arusha mchini Tanzania inatarajiwa kuanza Julai 18 mwaka 2019, ambapo vituo 238 vimetengwa.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu Julai 15,2019 Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Dk Wilson Mahela amesema taratibu zote muhimu za kuanza kwa shughuli hiyo zimekamika.

Mahela amesema ambao wanapaswa kujiandikisha ni vijana aliofikia umri wa miaka 18, wakazi ambao wamehamia jimbo la Arumeru Magharibi  na wale watahitaji kurekebisha majina yao.

Ofisa uchaguzi jimbo  la arumeru mashariki, Hadja  Mkumbwa akizungumza katika semina  ya waandikishaji katika daftari hilo, amewaka kufanyakazi kwa weledi na kuzingatia taratibu.

Amesema uandikishaji ni jambo la muhimu kwani wakikosea wao wameharibu juhudi zote za uandikishwaji na kupelekea kuharibu uchaguzi kwa ujumla.

"Hivyo tunawafundisha juu ya vitambulisho vilivyoharibika, fomu zitakazotumika pamoja na  kutumia mashine za BVR," amesema

Akizungumza mmoja mwandikishaji waliopewa semina Elias  Kizota amesema  mafunzo yameenda vizuri na kikubwa juu ya elimu waliyopata ni kuwa waadilifu katika utendaji kazi na kuwa na nidhamu.