Kanyasu atoa neno taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii

Thursday July 18 2019

By Anthony Mayunga, Mwananchi [email protected] co.tz

Serengeti. Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii ya nchini Tanzania zimeagizwa kushiriki maonyesho ya utamaduni kama njia ya kuinua utalii.

Kauli hiyo imetolewa leo Alhamisi Julai 18, 2019 na naibu Waziri wa wizara hiyo, Constantine Kanyasu katika uzinduzi wa maonyesho ya utamaduni ya Serengeti.

Amesema ushiriki wa taasisi hizo utachangia kusogeza utalii wa utamaduni kwa wananchi wengi.

"Vietnam wanapokea watalii milioni 15 kwa mwaka wanaokwenda kuangalia mambo ya asili, sisi (Tanzania) kama tungepata watalii milioni tano bajeti ya Taifa itakuwa imefidiwa,” amesema.

 

 

Advertisement

 

 


Advertisement