Abiria waliopata ajali ya treni Dodoma waondoka

Muktasari:

Abiria 1237 waliokuwa wakitokea mkoani Kigoma na kukwama jijini Dodoma baada ya mabewa mawili kupinduka na moja kuacha njia katika ajali ya kugongwa na lori, wameendelea na safari yao jana.

Dodoma. Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Patrobas Katambi amesema abiria wa treni ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) waliokwama kutokana ajali iliyotokea jana Jumanne karibu na Stesheni ya Dodoma wameondoka kwenda Dar es Salaam.

Ajali ambayo ilihusisha treni ya abiria 1,237 waliokuwa wakitoka Kigoma kwenda Dar es Salaam ilitokea baada ya lori kuiongonga treni hiyo.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatano Juni 19 2019, Katambi amesema abiria hao waliondoka jana Jumanne baada ya ukaguzi wa mabehewa ya treni hiyo kuonekana yanaweza kuendelea na safari.

“Faili lipo kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, taratibu zikikamilika atafikishwa mahakamani wakati wowote,” amesema Katambi