VIDEO: Adaiwa kujiua kwa kujichinja kwa kisu

Tuesday April 16 2019

Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha,Jonathan

Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha,Jonathan Shanna akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo.Picha na Filbert Rweyemamu 

By Filbert Rweyemamu, Mwananchi [email protected]

Arusha. Mkazi wa mtaa wa Simanjiro, kata ya Sombetini jijini Arusha, Lazaro Kiolori (53) anadaiwa kujiua kwa kutumia kisu kidogo chanzo kikielezwa kuwa ni ugomvi wa kifamilia.

Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Jonathan Shanna amesema leo Jumanne, Aprili 16, 2019 kuwa tukio hilo limeacha simanzi na mshtuko mkubwa kwa familia yake.

“Uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa chanzo cha marehemu kujitoa uhai wake ni mgogoro uliokuwepo kati yake na wake zake wawili ambao sitawataja majina yao kwa sasa na mwili upo katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru kwa uchunguzi zaidi,”amesema Shanna.

Amesema kuwa jeshi la polisi liliwahi kufika eneo la tukio na jitihada za kumwokoa hazikufanikiwa na kuwataka watu wenye msongo wa mawazo kuwatumia viongozi wa dini, wanafamilia na watalamu.

Advertisement