Alaf wazindua shindano la mpigapicha bora utunzaji wa maji

Muktasari:

  • Kampuni ya vifaa vya ujenzi nchini Tanzania ya Alaf imezindua shindano la upigaji picha zinazohamasisha utunzaji wa vyanzo vya maji na mshindi atajinyakulia Sh6.8 milioni

Dar es Salaam. Kampuni ya vifaa vya ujenzi nchini Tanzania ya Alaf imezindua shindano la upigaji picha zinazohamasisha utunzaji wa vyanzo vya maji na mshindi atajinyakulia Sh6.8 milioni.

Shindano hilo litakalohusisha raia wa Tanzania, Kenya, Uganda limezinduliwa leo Ijumaa Julai 19, 2019  na kupewa jina la Safal eye in the world lenye kauli mbiu ya kila tone moja lina thamani.

Mkuu wa masoko wa Alaf,  Isamba Kasaka amesema, "Katika mitandao ya kijamii tunatangaza namna ya kutuma picha hizo washiriki wengi watapata zawadi. Wa kwanza atapata Sh6.8 milioni, wa pili Sh4.5 milioni, watatu Sh2.2 milioni na mpiga picha bora Sh1.1 milioni. Kuna watakaopata zawadi ya kamera na nyinginezo.”

Katibu tawala wa Wilaya ya Kinondoni, Stella Msofe amesema hamasa hiyo ni nzuri kwa kuwa italeta  matokeo chanya kwa kuzingatia umuhimu wa maji katika shughuli za kila siku.