Anayekabiliwa na kesi ya mauaji jela miaka miwili kwa kutoroka mahakamani

Thursday February 14 2019

By Anthony Mayunga, Mwananchi [email protected]

Serengeti. Mtuhumiwa wa kesi ya mauaji aliyetoroka mahakamani jana Jumatano Februari 13, 2019 amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela.

Emmanuel Mase anayekabiliwa na kesi ya mauaji namba 23/2018, jana alitimua mbio katika mahakama ya Wilaya ya Serengeti. Hata hivyo kabla ya kufika mbali wananchi walimkamata.

Mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo, Ismael Ngaile, mwendesha mashtaka wa Serikali,  Renatus Zakeo leo Alhamisi Februari 14, 2019 amesema mshtakiwa anakabiliwa na kosa moja la jinai.

Zakeo amesema katika kesi ya jinai namba 220/18, mshtakiwa huyo kosa lake ni kutoroka chini ya ulinzi wa mahakama.

Akisoma hukumu hiyo, hakimu Ngaile amesema kosa alilotenda mshtakiwa huyo ni kinyume na kifungu cha 116 na 35 cha Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 mapitio 2002, kwamba atatumikia adhabu ya miaka miwili jela huku akiendelea na kesi yake ya mauaji.


Advertisement