Aneth Kushaba aachia wimbo wa kuhamasisha amani nyakati za chaguzi

Monday June 24 2019

 

By Tumaini Msowoya, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Mwanamuziki aliyewahi kutikisa katika bendi mbalimbali nchini Tanzania ikiwamo Machozi, Skylight na B. Band inayomilikiwa na Banana Zoro ameachia video mpya ya muziki wa Injili inayokuja kwa jina la ‘Peace’.

Peace ni wimbo wa pili wa Injili kuachiwa na mwanadada huyo ambaye awali aliachia ‘Haleluya’.

Aneth Kushaba alia kufahamika vyema kwa wapenzi wa burudani kupitia shindano la kusaka na kuibua vipaji, linalojulikana kama Tusker Project Fame (TPF) mwaka 2010 na sasa  sasa anaimba  kupitia band yake ya Star.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu Juni 24,2019 wakati akiutambulisha wimbo wake mpya, Aneth amesema ameimba ‘Peace’ kuendelea kuhamasisha amani nchini hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

“Nchi inapitia mengi kwa hiyo wimbo huu wa amani ulinijia na Mungu aliamua kuongea na mimi kuhusu jambo hili muhimu, wimbo upo kwenye video na tayari unapatikana Youtune,” alisema Aneth.

Kuhusu kuhamia kwenye muziki wa Injili, Aneth ambaye pia anamiliki bendi yake amesema hakuwa na uwezo wa kutetea nyimbo za awali alizokuwa akiimba kwa sababu hazikuwa na uhalisia wa maisha yake.

Advertisement

“Kama nikisema nakupenda, nampenda nani? Sijaolewa na kama boy friend ‘rafiki wa kiume’ nitawaimba wangapi? Kwa hiyo sikuwa na weza kutetea ujumbe wake nikiulizwa kwa nini nimeimba hivyo ila sasa hivi naweza kutetea kile ninachoimba,” amesema.

Rebecca Marope kutoka nchini Afrika Kusini ndiye mwimbaji wa muziki wa Injili anayefurahia ‘role model’ kutokana na uimbaji wake mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Mbwana Ally Samatta akiwa mchezaji anayemkubali.

Bendi yake kwa sasa inafanya kazi katika hoteli mbalimbali ikiwamo Serena na Slipway na yupo mbioni kuachia albamu yake, lakini kwanza ameamua kujitambuliwa kwa video hiyo aliyoifanya chini ya mikono ya mwandaaji  Dibro.

Advertisement