Arnold Schwarzenegger apigwa teke Afrika Kusini

Muktasari:

  • Nyota wa Hollywood, Arnold Schwarzenegger amepigwa teke na shabiki hadharani katika hafla moja nchini Afrika Kusini na amesema hatomfungulia mashtaka mtu aliyemshambulia.

Pretoria, Afrika Kusini. Nyota wa Hollywood, Arnold Schwarzenegger amepigwa teke na shabiki hadharani katika hafla moja nchini Afrika Kusini na amesema hatomfungulia mashtaka mtu aliyemshambulia.

Schwarzenegger alituma ujumbe wa twitter kwa mashabiki wake zaidi ya milioni nne akisema: “Nilidhania kwamba nilikuwa nimesukumwa na watu waliojaa katika hafla hii, ambacho ni kitu cha kawaida.”

“Niligundua kwamba nilipigwa teke nilipoona kanda ya video kama vile nyiny.”

Akijibu ujumbe wa twitter kutoka kwa mashabiki wake siku ya Jumapili, alisema hatomfungulia mashtaka mshambuliaji wake.

''Tuna michezo 90 hapa Afrika Kusini na wanamichezo 24,000 wa kila umri, kitu kinachotupatia moyo kushiriki. Tuwaangazie wanariadha hawa,” aliandika katika mtandao wake wa Twitter.

 

Kanda ya video iliyosambaa mitandaoni ilionyesha kuwa nyota wa Schwarzenegger akishambuliwa katika hafla hiyo kwa mujibu wa BBC

Gavana huyo wa zamani wa jimbo la California mwenye umri wa miaka 71 alikuwa akizungumza na mashabiki wake wakati wa mashindano ya kuruka kamba katika hafla yake ya michezo barani Afrika wakati mtu mmoja alipompiga teke kutoka nyuma.

Mshambuliaji huyo baadaye anaonekana akishikwa na kudhibitiwa baada ya kisa hicho.

Schwarzenegger aliwashukuru mshabiki wake katika mtandao a twitter waliotaka kumjulia hali na kusisitiza kuwa hakuna cha kujali.

Nyota huyo wa The Terminator alikaribia kuanguka baada ya teke hilo, huku mshambuliaji wake akianguka chini ambapo alikamatwa na walinzi.

Mtu huyo baadaye alikabidhiwa kwa maofisa wa polisi kwa mujibu wa wenyeji wa hafla hiyo.