Baba Diamond alivyoibua shangwe ukumbini

Monday July 8 2019

By Nasra Abdallah, Mwananchi

Dar es Salaam. Abdul Juma ambaye ni baba wa msanii wa Tanzania, Diamond Platnumz, amejikuta akishindwa kuzuia hisia zake na kuwakumbatia mzazi mwenzake, Sandra jukwaani na kuzua  shangwe.

Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia leo Jumatatu Julai 8, 2019 katika sherehe za kuzaliwa kwa mama yake mzazi, Sandra pamoja na mpenzi wake, Tanasha Donna zilizofanyika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam nchini Tanzania.

Juma alijikuta akifanya kitendo hicho pale msanii Abdul Misambano alipoimba wimbo wa 'Asu' maalum kwa ajili ya mama Diamond ambaye alieleza kipindi alichokuwa akiimba ndio walikuwa mashabiki zake.

Kibao hicho kilipoanza kupigwa kwa kutumia vyombo vya muziki vya live vilivyokuwepo ukumbini hapo, kilimuamsha Abdul kwenye kiti na kwenda kucheza pamoja na mzazi mwenzake waliomzaa Diamond.

Abdul hakuishi kucheza na mzazi mwenzake peke bali alihamia kwa mme wa mama Diamond anayeitwa

Mwananchi ilizungumza na Abdul baada ya kumaliza kucheza muziki na kuwakumbatia wawili hao bila kuwa na hofu akisema, “kila mtu sasa hivi ana maisha yake na hapa tupo kwa ajili ya furaha na kupongeza mzazi mwenzangu na mkwe wangu kuongeza mwaka mwingine hivyo sioni shida."

Advertisement

Advertisement