Balozi wa Zambia nchini Kenya afariki

Muktasari:

  • Alipopata ajali alikuwa ameambatana na balozi wa Botswana nchini Kenya Duke Lephoko

Nairobi,Kenya. Balozi wa Zambia nchini Kenya Brenda Muntemba-Sichilembe, amefariki dunia jijini Nairobi baada ya kupata ajali.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje Macharia Kamau, amesema leo Jumatano Machi 20, 2019 kwamba balozi huyo alipoteza maisha baada ya kupata ajali ya gari barabara ya Machakos.

Amesema Mutemba (49), alipoteza maisha akipatiwa matibabu Hospitali ya Nairobi baada ya ajali iliyotokea wiki tatu zilizopita.

Kamau amesema balozi huyo alipata ajali Februari 26, 2019 eneo la Lukenya barabara ya Mombasa baada ya gari lake  kugongana na gari kubwa la mizigo.