Basi la Buffalo lapata ajali, abiria 47 wanusurika kifo

Muktasari:

Basi la Kampuni ya Buffalo linalofanya safari kati ya Arusha na Dar es Salaam nchini Tanzania limepata ajali wilaya ya Handeni mkoani Tanga. Hakuna vifo wala majeruhi.

Handeni. Abiria 47 waliokuwa wakisafiri kutoka Mkoa wa Arusha kwenda Dar es Salaam nchini Tanzania wamenusurika kifo baada ya basi walilokuwa wakisafiria mali ya kampuni ya Buffalo kugongana na gari ndogo na kupinduka.

Akizungumzia ajali hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, Godwin Gondwe amesema tukio hilo limetokea leo Jumatano Agosti 14,2019  katika kijiji cha Kwekwale na hakuna kifo chochote kilichotokea.

Amesema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi la Buffallo, Innocent Mauki kutoka kuyapita magari mengine mawili yaliokuwa mbele yake huku eneo husika likiwa na alama za kukataza gari kumpita mwenzake.

"Naliagiza jeshi la polisi kumtafuta dereva wa hili basi halafu ashitakiwa kwa kosa la ku over take sehemu ambayo alama haziruhusu kufanya hivyo," amesema Gondwe.

Lucas Karoli dereva wa gari ndogo yenye namba T 706 DPE amesema aliona dereva wa basi hilo akijaribu kuyapita magari mawili yaliokuwa mbele yake huku alama zikiwa haziruhusu na ndio akaligonga gari lake upande wa kulia.

Abiria waliokuwepo kwenye ajali hiyo wametafutiwa gari nyingine na kuendelea na safari.

T: Basi la Buffalo lapata ajali, abiria 47 wanusurika kifo

S: Basi la Kampuni ya Buffalo linalofanya safari kati ya Arusha na Dar es Salaam nchini Tanzania limepata ajali wilaya ya Handeni mkoani Tanga. Hakuna vifo wala majeruhi.

Rajabu Athumani, Mwananchi