Bendi ya masister ya Rock&Roll kutumbuiza mbele ya Papa Francis

Muktasari:

Pamoja na kundi hilo, linalojiita Siervas au Watumishi lina wanamuziki 11 na lenye makazi yake ni nchini Peru, kuimba muziki wa rock, wasanii wake hawahusudu matumizi ya dawa za kulevya au masuala ya kujamiiana.


Si jambo la kawaida kwa waumini wa Kanisa Katoliki, lakini ndivyo itakavyokuwa wakati kundi la watawa linalopiga muziki wa Rock&Roll litakapotumbuiza mbele ya kiongozi wa kanisa hilo duniani, Papa Francis.

Kundi hilo la Masister, ambalo tayari limevuta mashabiki milioni kwenye mtandao wa YouTube na lina nyimbo zilizoshika chati Spotify na iTunes, litapata nafasi hiyo ya kutumbuiza mbele ya Papa na maelfu ya wafuasi wa dini hiyo wiki ijayo.

Kundi hilo linaweza kuwa la muziki wa huo maarufu duniani, lakini watawa hao hawana tabia za wasanii wa muziki huo, na pia kujamiiana na matumizi ya dawa za kulevya si sehemu ya maisha yao kama ilivyo kwa wanamuziki wengine wa Rock&Roll.

Watawa hao kumi na moja wanaojiita Madada wa watumishi wa Mpango wa Mungu (Sisters of the Sevants of Plan of God), wanapiga muziki huo ukiwa katika utamaduni wao na sauti zilizopangiliwa vizuri, tofauti na nyota wengine wa ROck&Roll ambao huimba kwa kelele na ala kupigwa mithili ya vurugu.

"Sisi bado ni wasichana," anasema Sister Ivonne, mwenye umri wa miaka 37 wa kundi hilo ambalo wanamuziki wake wengine wanatoka nchi za Chile, Japan, Ecuador, China na Costa Rica.

"Hii ni njia nyingine ya kutuma ujumbe wa injili, kuonyesha nguvu yetu -- hii ni kusema pia ni muziki ambaop tunaupenda, unaonyesha mambo mengi kuhusu sisi ni nani."

Kundi hilo likitumia jina la "Siervas" au Watumishi, linapiga nyimbo za Kikristo ambazo zinaonekana hazitofautiani na nyimbo za nyingine za rock.

Lakini muonekano ni tofauti kutokana na mavazi ya watawa hao.

Ikiwa na video zipatazo sita kwenye YouTube, Siervas imeweza kuvuta mashabiki wengi duniani, ikituma ujumbe wa "upendo, furaha na tumaini".

Video yao ya "Trust in God", ambayo inawaonyesha watawa waki wakiiwa juu ya ghorofa refu jijini Lima, ilisambaa kwa haraka na kutazamwa na karibu watu milioni mbili.

Na sasa kundi hilo lenye makazi yake nchini Peru litatumbuiza katika sherehe ya Siku ya Vijana Duniani, wakati vijana wa Kanisa Katoliki watakapokutana Panama ambako Papa Francis atakuwepo.

Ni ujumbe gani ulio nyuma ya muziki wqao? "Tunataka kuwafikia watu wengi kadri iwezekanavyo, na kama Papa atakuwepo katika hilo (tamasha) tutaridhika zaidi," alisema Ivonne, ambaye huandika sehemu kubwa ya mashairi ya nyimbo zao. AFP