Boda boda kupatiwa ahueni ya adhabu

Muktasari:

Serikali ya Tanzania imetoa waraka kueleza makosa na adhabu wanazotakiwa kutozwa wanapokamatwa watu wa bodaboda.


Dodoma.Wizara ya Mambo ya Ndani wametoa waraka unaowapa nafuu waendesha bodaboda ili kuwapunguzia adhabu za makosa barabarani, Bunge limeelezwa leo Juni 13,2019.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amesema wizara ilishaandika waraka na kuupeleka makao makuu ya nchi ili watekeleze.

Ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Bunda, Mwita Getere aliyeuliza kwa niaba ya Mbunge wa Musoma Mjini (Wote wa CCM) kuhusu namna Serikali ya Tanzania itakavyoweza kutofautisha adhabu ya waendesha bodaboda na ile ya magari makubwa kulingana na vipato vyao.

Masauni amekiri kuwa iko haja ya kutofautisha adhabu kutokana na vipato kwa vyombo hivyo ukilinganisha na magari.