Boris Johnson azidi kung’ara kinyang’anyiro cha kumrithi May

Thursday June 20 2019

 

Londan, Uigereza. Waziri wa zamani wa mambo ya nje nchini Uingereza, Boris Johnson ameongoza katika awamu ya tatu ya mchujo wa wagombea wanaowania kuchukua uongozi wa chama cha Conservative.

Johnson amepata kura kura 157 kati ya 313 zilizopigwa na wabunge wa chama hicho leo Alhamisi June 21, huku nafasi ya pili ikifuatiwa na waziri wa mazingira, Michael Gove aliyepata kura 61.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ungereza (BBC), nafsi ya tatu ilichukuliwa na waziri wa mambo ya nje wa sasa, Jeremy Hunt aliyepata kura 59.

Kwa upande wake waziri wa mambo ya ndani, Sajid Javid alipata kura 34 hivyo kuondolewa katika kinyang’anyiro hicho.

Ijuma June 7, Theresa May, alijiuzulu uongozi wa Conservative ikiwa ni mwezi mmoja tangu kutangaza kuachia nafas ya uwaziri mkuu wan chi hiyo.

Julai mwaka huu wanachama wote wa Conservative  wanatarajia kuwapigia kura wagombea wawili ili kupata mwenyekiti wa chama na baadaye waziri mkuu wananchi hiyo.

Advertisement


Advertisement