Bunge la Marekani lapinga lamgomea Trump

Muktasari:

Ni kuhusu mpango wake wa mauzo ya silaha kwa Saudi Arabia.

Washington, Marekani. Bunge la Marekani limepiga kura ya kuzuia mauzo ya silaha ya kiasi cha dola bilioni 8.1 kwa Saudi Arabia na washirika wengine.

Hatua hiyo huwenda ikamlazimisha Rais Donald Trump kutumia kura yake ya turufu kupinga hoja hio.

Katika kura hiyo wabunge hao waliidhinisha mambo matatu ambayo yatazuia mauzo tata yaliyotangazwa na Rais Trump mapema mwaka huu chini ya hatua za dharura.

Maazimio hayo ya kuzuia mauzo ya silaha tayari yameidhinishwa na Baraza la Seneti na sasa yanakwenda katika Ikulu ambako Trump anatarajiwa kutumia kura yake ya turufu kwa mara ya tatu tangu alipoingia madarakani.

Kwa mujibu wa wabunge hao, mauzo hayo ya silaha yanaweza kuchochea zaidi vita vya Yemen ambako Saudi Arabia inaongoza muungano wa kijeshi unaoungwa mkono na Marekani katika mapambano dhidi ya waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran.