Chadema Arumeru washtushwa Nassari kung’olewa ubunge

Muktasari:

  • Chadema Arumeru yashtushwa baada ya Nassari kung'olewa ubunge, yataka utulivu kwanza kwa wanachama wake wakati suala hilo likishughulikiwa

Arumeru. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Jimbo la Arumeru Mashariki kimeeleza kupokea kwa mshtuko taarifa za kuvuliwa ubunge, Joshua Nassari na Spika wa Bunge, Job Ndugai na kimewataka wanachama wake kutulia wakati suala hilo linashughulikiwa kisheria.

Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Meru, Gadiel Mwanda amesema sababu zilizotolewa na Spika kuwa Nassari ameondolewa kwa kutohudhuria vikao vitatu mfululizo bila taarifa zimewaumiza wengi.

"Suala hill limepokelewa katika mitazamo tofauti, wapo walioumia kwa kuamini kuwa Mhe Nassari anaonewa kwa kuhukumiwa pasipo kupewa nafasi ya kusikilizwa huku wakiamini kuwa alitoa taarifa kwa barua aliyoituma kwa Spika kupitia Email rasmi ya Bunge Februari 29, 2019. Lakini wapo walioumia kwa kuamini kuwa alifanya uzembe," amesema.

Amesema Chadema jimbo la Arumeru Mashariki inawapa pole wanachama  wote na wananchi kwa ujumla kwa lililotokea na kwamba inawasihi kuwa watulivu,wastahimilivu na wakomavu katika kipindi hiki kigumu.

Mwanda amesema Chadema Jimbo kwa kushirikiana na Nassari Mbunge wana fanya mawasiliano na uongozi wa Chama Taifa pamoja na wanasheria  kwa mashauriano na baada ya hapo watawafahamisha rasmi muda na mahali ambapo Mhe,Nassari na uongozi wa Chama watafanya mkutano na vyombo vya habari