China kushirikiana na Afrika kulinda urithi wa dunia

Thursday May 30 2019
CHINA PIC

Dar es Salaam. Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (Unesco) limeandaa semina ya siku mbili ya kuimarisha ushirikiano baina ya Afrika na China kulinda urithi wa dunia.

Mkutano huo utakaofanyika jijini Paris, Ufaransa kati ya Juni 3 na 4, na kufunguliwa na mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo, Audrey Azoulay, ujadili namna ya kulinda vituo vya urithi wa dunia, usajili wa vituo vipya, ajira na namna ya kuwawezesha vijana. Vilevile, mkutano huo utaangazia uongezwaji wa vituo kwenye orodha inayotambuliwa na Unesco.
kwa sasa, Afrika ina vituo 95 kati ya 1,052 vinavyotambulika. Kati ya vituo hivyo, 814 ni vya utamaduni, 203 ni vya asili na 35 mchanganyiko. Kati ya vituo hivyo, saba vipo Tanzania ambavyo ni michoro ya mapangoni Kondoa (2006), magofu ya kale Kilwa Kisiwani na Songo Mnara (1981), Mji Mkongwe Zaznibar (2000), Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro (1987), Hifadhi ya Taifa  Selous (1982), hifadhi ya Taifa Serengeti (1981) na Hifadhi ya Taifa Ngorongoro (1979 na 2010).
“Vituo 95 vilivyopo Afrika ni chini ya asiliimia tisa ya vyote vinavyotambulika. Hata hivyo, theluthi moja ya vivutio vilivyo katika hatari ya kutoweka ni duniani vipo Afrika. Mkutano huu utaimarisha ushirikiano wa Afrika na China kulinda vituo vilivyopo,” amesema Azoulay.

Advertisement