Chumba Uwanja wa Ndege Dar chateketea kwa moto

Muktasari:

  • Moto wa ghafla wateketeza vifaa na nyaraka za ofisi zilizopo katika jengo la Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Terminal 3

Dar es Salaam. Chumba kimojawapo cha ofisi kilichopo katika jengo la Uwanja wa Ndege  wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)  jengo la Terminal 3, kimeungua kwa moto ambao bado chanzo hakijajulikana.

Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto JNIA, Maria Kulaya ameiambia Mwananchi leo Jumapili Machi 24, 2019 kuwa tukio hilo lilitokea jana jioni baada ya moto huo kuzuka ghafla katika chumba cha ofisi hiyo kinachotumiwa na wakandarasi

Kulaya  amesema ingawa haukuwa na madhara kwa kuwa jeshi hilo liliwahi baada ya kupewa taarifa, lakini baadhi ya vifaa na nyaraka zilizokuwemo kwenye chumba hicho zimeteketezwa na moto huo.

“Kamishna Jeneral wa Zimamoto, Tobias Andengenye alitembelea leo hapa na tayari tumeshaanza uchunguzi ili kubaini chanzo cha moto huu. Tutoa taarifa rasmi baada ya kukamilika kwa mchakato huu,”amesema.