TAMTHILIA YA SULTAN: Colimba Malecela,mhitimu wa Tasuba anayenakilisha sauti ya Hadim Pasha

Wednesday January 16 2019

 

Akiwa na umri wa miaka 26, Sultan Suleyman alianza mbio za kuitengeneza himaya yake ya Ottoman akitaka iwe kubwa kuliko ya Alexander the Great. Utawala wake wa miaka 46 ulihitajika ulimwenguni kote akiwa na Pargali Ibrahim.

Kuhusu Hadim Pasha

Nafasi ya Hadım Suleiman Pasha imeigizwa na Ibrahim Raci Oksuz ambaye alipata umaarufu kupitia filamu ya Baba Nerdesin Kayboldum iliyotoka mwaka 2018.

Pia alishawahi kucheza filamu ya Yesil Deniz ya mwaka 2014.

Colimba Malecela

Ni mwigizaji wa filamu, tamhtilia pamoja na sauti.

Katika tamthilia ya Sultan ananakili sauti ya Kassi Pasha, aliyefukuzwa kazi kwa kosa la kwenda kinyume na maadili ya kazi ya Uwaziri.

Anasema anachoshukuru tofauti na watu wengine yeye kasomea kazi ya uigizaji na ana shahada kutoka Taasisi ya Sanaa Bagamoyo (TasuBa) katika masuala ya uigizaji, kucheza ngoma na sanaa za maonyesho.

Malecela anasema anashukuru pamoja na kufanya kazi na vikundi visivyopungua 15, amejifunza mambo mengi ambayo asingependa yatokee kwenye kazi zake za sanaa.

Aliyataja mambo hayo kuwa ni pamoja na mnapokuwa kwenye kundi hata kama ni kiongozi usiwe msemaji na mwamuzi wa kila jambo, kwa madai waliofanya hivyo wamekuwa wakiharibu hata kazi wanayoifanya.

“Utakuta kwa kuwa mtu ni kiongozi, basi anamchezesha mtu wake nafasi ambaye hata hastahili na hivyo kama ni filamu au tamthilia inakosa uhalisia kwa kuwa kama alitakiwa awekwe mtu mnene anawekwa mwembamba kisa tu ni mtu wake wa karibu, ”anasema

Pia anasema uvumilivu wake katika tasnia ya uigizaji ndio umemfikisha hapo kwani aliwahi kwenda na watayarishaji eneo la kupigia picha za filamu na hakupangwa, aliishia kubeba mabegi lakini hakukata tamaa.

“Elimu haimtupi mtu, nimesoma na ninaona mambo yanafunguka ikiwamo kupata nafasi hii ya kunakilisha sauti, ”anasema.

Advertisement