VIDEO: Diamond awazawadia magari ya kifahari mama yake, Tanasha

Monday July 8 2019

 

By Nasra Abdallah, Mwananchi

Dar es Salaam. Msanii maarufu wa Tanzania, Diamond Platnumz amewazawadia magari ya kifahari mama yake mzazi, Sandra pamoja na mpenzi wake, Tanasha Donna katika siku yao ya kuzaliwa jana Jumapili Julai 7, 2019.

Diamond aliwakabidhi wawili hao katika iliyomalizika usiku wa kumakia leo Jumatatu sherehe aliowaandalia wawili hao iliyofanyika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam nchini Tanzania na kuhudhuriwa na watu mbalimbali.

Gari hizo aina ya Landcruser Prado, zinaelezwa kila moja kuwa na thamani isiyopungia zaidi ya Sh160 milioni.

Diamond aliwakabidhi wawili hao gari hizo saa 8:00 usiku wa kuamkia leo baada ya kuisha kwa sherehe hizo ambapo magari hayo yaliegeshwa nje.

Magari hayo yalibandikwa namba yakisomeka majina ya 'mama Dangote' ambaye ni mama yake mzazi na lile la mpenzi wake likiandikwa 'Tanasha.'

Wa kwanza kukabidhiwa gari alikuwa mama yake mzazi aliyemfungilia mlango kisha akahamia kwa Tanasha.

Advertisement

Hata hivyo wakati wa kuondoka Tanasha ndiye aliendesha gari hilo, wakati lile la mama yake liliendeshwa na mume wake, Shamte ambako nyuma walipanda ndugu mbalimbali waliohudhuria sherehe hizo.

Mbali ya kupata zawadi hiyo ya gari, awali wakiwa ukumbini wawili hao walipewa makasha saba ambayo kulikuwa na zaidi mbalimbali kila mmoja alitakiwa kuchagua moja.

Katika kuchagua huko, Tanasha alishinda nyumba huku mama yake mzazi, Sh10 milioni ambazo hata hivyo ilielezwa watagawana milioni tano tano na Tanasha.

Advertisement