VIDEO: Diamond azungumzia kufunga ndoa na Tanasha

Monday July 8 2019

By Nasra Abdallah, Mwananchi

Dar es Salaam. Msanii maarufu nchini  Tanzania, Diamond Platnumz amesema hakuna mahali alitangaza kufunga ndoa na mpenzi wake, Tanasha Donna.

Badala yake amesema anachojua aliwaambia mashabiki zake kwamba atafanya sherehe ya kuzaliwa kwa mama yake, Sadra pamoja na mpenzi wake Tanasha ambaye ni raia wa Kenya.

Katika mahojiano na Mwananchi, leo Julai 8,2019, Diamond amesema hiyo swali amekuwa akiulizwa mara kwa mara lakini ukweli ni kwamba hajatangaza kufanyika kwa ndoa.

Alipoulizwa siku ya leo aliyoiandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa leo angemaliza kabisa, amesema ilikuwa ni katika kupamba sherehe hizo lakini sio kwamba kuna harusi.

"Katika sherehe kuna mbwembwe nyingi, ninachoshukuru ni shughuli ya wapendwa wangu hawa umeenda vizuri na kuisha salama,” amesema Diamond.

"Nawashukuru watu wote waliojitokeza kunipa sapoti katika kusherekea siku hii muhimu kwangu," amesema.

Advertisement

Kuhusu harusi amesema siku ikifika atatangaza na kwa kuwa yeye ni mtu maarufu watu watajua tu.

Advertisement