Dudu Baya akiri kumpiga makofi Gigy Money

Muktasari:

  • Amesema alimshushia kipigo  kwa sababu alimkosea adabu mbele ya mtoto wake.

Msanii wa Bongo Fleva, Godfrey Tumaini maarufu kwa jina la Dudu Baya, amekiri kumpiga msanii  mwenzake Gigy Money.
Gigy Money ambaye jina lake halisi ni Gift Stanford akihojiwa na kituo cha Wasafi TV jana Mei 20, alieleza kuwa Dudu Baya alimpiga baada ya kumtaka kimapenzi na kumkataa.
Leo Mei 21, akizungumza na Mwananchi, Dudu Baya amekiri kumpiga msanii huyo aliyepata umaarufu kupitia wimbo Nampa Papa.
Akielezea tukio zima lilivyokuwa , amesema ilikuwa mwishoni mwa mwaka jana walipokuwa katika tamasha la Wasafi Festival mkoani  Mwanza ambapo Gigy alimtukana matusi ya nguoni  mbele ya mtoto wake wa aliyemtaja kwa jina la Maria.
Amesema Gigy alimwambia ana uume mkubwa jambo ambalo liliamsha hasira zake kwa kuwa mbali ya kwamba haileti picha nzuri kwa jamii, pia kamdhalilisha mbele ya mtoto wake amvaaye swali naye alitaka kunipiga wakamzua.
"Hii tukio ni kweli na nilimpiga mbele ya Hadija Kopa na Jackline Wolper ambao walimshuhudia akiporomosha matusi na kwa uhakika kuhusu tukio hilo waulizeni hata wao," amesema msanii  huyo aliyewahi kutamba na wimbo 'Nakupenda Tu'.
Alipoulizwa kwa nini hayo yote hayakuelezwa kipindi hicho cha tamasha, Dudu amesema waliamua kupotezea kwa kuwa hawakuona kama ilikuwa na tija kwa jamii na kuongeza kuwa waligundua siku hiyo Gigy alitaka kutafuta 'kick' jambo ambalo hawakumpa nafasi.
Wakati kuhusu kumtaka kimapenzi, amesema Gigy ndiye alimtaka, lakini alishampa masharti ili aweze kuwa mpenzi wake anapaswa kubadilika kitabia ikiwemo kuvaa mavazi yenyewe staha na kuacha kutukana ovyo.