Fikra za usawa kwa wote na uvumbuzi kwa ajili ya mabadiliko

Tuesday March 19 2019

 

Kila mwaka ifikapo Machi 08, ulimwengu huja pamoja na kusherehekea sikukuu ya wanawake duniani.

Hapa tunatambua malezi, upendo usiokwisha, kafara na michango mingine mbalimbali ambayo imekuwa ikiletwa na mwanamke katika kuhakikisha dunia inakuwa bora na mahali salama na amani kwa kila binadamu.

Katika kuendeleza juhudi zake za kumtambua na kumsherehekea mwanamke, Vodacom ilizindua kampeni yenye kauli mbiu, FIKRA ZA USAWA NA UVUMBUZI KWA AJILI YA MABADILIKO, ikiwa na lengo la kuwaendeleza hasa wasichana walio shuleni na kuwapa nyenzo na dira katika maisha yao ya baadae.

Kampeni ilizinduliwa rasmi na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Hisham Hendi.

Advertisement