Gari la ‘mahakama inayotembea’ lazinduliwa Mwanza

Friday July 12 2019

Gari maalum itakayotumika kutoa huduma ya

Gari maalum itakayotumika kutoa huduma ya Mahakama inayotembea mkoani Mwanza. Mahakama hiyo imezinduliwa Julai 12, 2019 na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Sam Rumanyika. Picha na Johari Shani 

By Johari Shani, Mwananchi [email protected]

Mwanza. Jaji mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mwanza, Sam Rumanyika amezindua gari maalumu la Mahakama inayotembea litakaloweza kusaidia usikilizwaji wa mashauri katika Mkoa wa Mwanza.

Uzinduzi huo umefanyika leo Julai 12, 2019 katika hafla inayoendelea eneo la viwanja vya Mahakama Kuu jijini Mwanza.

Jaji Rumanyika amesema gari hilo litaanza kutoa  hudumia kata za Buswelu, Igoma na Buhongwa lengo likiwa ni kurahisisha upatikanaji wa huduma za mahakama, kufungua mashauri, wananchi kupata tarehe za mwendelezo wa kesi  na kupata nakala za hukumu katika kipindi kifupi kisichozidi wiki moja.

Advertisement