Halima Mdee aitwa Polisi kwa mahojiano

Muktasari:

Mbunge wa Kawe (Chadema), Halime Mdee leo Jumamosi amekwenda Polisi Oysterbay kuitikia wito wa Kamanda wa Upelelezi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni (RCO).

Mdee amesema hafahamu ameitwa kwa sababu zipi

Dar es Salaam. Mbunge wa Kawe (Chadema), Halime Mdee ameitikia wito wa Polisi Kinondoni jijini Dar es Salaam aliotakiwa kufika leo Jumamosi Februari 23,2019.

Mdee kupitia akaunti yake ya Twitter ameandika, “Nimepata wito wa kuitwa Polisi Oysterbay kwa mahojiano.”

“Mpaka sasa sababu ya wito ni nini. Ngoja tujongee.”

Baada ya ujumbe huo, Mwananchi limezungumza na Mdee ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) kujua kama amekwisha kufika na kujibu kwa ujumbe mfupi wa maandishi, “Niko kwa RCO. Nimepokelewa, Namsubiri.”

 

Endelea  kufuatilia Mwananchi kujua kinachojiri