Halmashauri ya wilaya Handeni wachaguana

Thursday May 16 2019

Baadhi ya madiwani wa halmashauri ya wilaya ya

Baadhi ya madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Handeni wakiendelea na kikao chao cha kawaida cha kijadili mambo mablimbali ya maendeleo ya halmashauri hiyo kinachofanyika leo Mei 16.Picha na Rajabu Athumani 

By Rajabu Athumani, Mwananchi [email protected]

Handeni. Diwani wa Kwamgwe Halmashauri ya Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, Sharifa Abebe, amechaguliwa kuwa makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo kuziba nafasi iliyokuwa wazi kwa miezi miwili.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika leo Alhamisi Mei 16, 2019 mwenyekiti wa halmashauri hiyo,  Mustafa Beleko amesema kwa pamoja baraza limempitisha kuwa makamu mwenyekiti.

Baleko amesema wajumbe walikuwa 26 wote walipiga kura ya ndio kumchagua mshindi.

"Hii nafasi ya makamu mwenyekiti ilikuwa wazi kwa miezi miwili sasa, hivyo tumeshauri ufanyike uchaguzi, CCM ndio wameleta mgombea na wapinzani ambao ni Chadema hawakuleta mgombea,” amesema.

 


Advertisement