Hoja ya Waziri Mpango kuhusu CCM ndiyo pekee yawagawa wananchi

Muktasari:

  • lhamisi iliyopita ya Juni 13, 2019, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango akiwasilisha mapendekezo ya Bajeti ya Serikali ya mwaka 2019/20, pamoja na mambo mengine alisema katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Oktoba 2019, moja ya sifa ni mgombea awe anatokana na Chama cha Mapinduzi (CCM)

Dar es Salaam. Hoja ya sifa ya mgombea wa uchaguzi wa serikali za mitaa awe anatokana na CCM imeibua mjadala kwenye mitandao wengi wakihoji kama huo utakuwa uchaguzi huru na wa haki.

Mjadala huo katika mitandao ya Instagram na facebook inayoendeshwa na Mwananchi, inatokana na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango kueleza sifa hiyo Alhamisi ya Juni 13, 2019 bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha bajeti ya serikali ya mwaka 2019/20.

Kama ilivyotokea bungeni baada ya kutoa kauli hiyo kwa wabunge wa pande zote kushangilia huku wengine wakisimama na kugonga meza huku wakionyesha mshangao wa kauli hiyo, ndivyo imekuwa katika mitandao hiyo ya kijamii ambapo wananchi wamehoji mbalimbali.

Wananchi hao wamehoji hayo baada ya habari inayohusu sifa hiyo aliyoitoa Dk Mpango ilipowekwa ambapo burhansaid83 anasema, “hivi huku tunakokwenda ndio mbele au tunarudi tulikotoka!!” huku kindungwajr akihoji, “sasa wakiwa CCM wote kuna haja gani yakua na uchaguzi.”

jog_fisa_mwapasi amesema, “nitakua nipo ndotoni siyo kweli hii.” Naye omary.mbena

amechangia hoja hiyo akihoji, “kwa hiyo nchi sio ya vyama vingi tena” naye
Issa Mwasumbi anasema, “Huo utakuwa uchaguzi au kubadilisha viongozi tunachokitafuta tutakipata.”                     

mjadala umeendeela ambapo tiko_dm amesema, nchi inatia aibu sana hii. Sasa vyama vingi maana yake huku mwasomolamichael amesema vyama vingi viko wapi? Kama vipo kauli hiyo ina maana gani?

evojo2016 amesema kama Serikali imepanga hivyo sioni haja ya kupoteza fedha kwa ajili ya uchaguzi CCM iwateue tu hizo pesa zikasaidie maeneo mengine. Hi itasaidia sana kupatikana kwa fedha za kukamilisha miradi mbalimbali ya huduma za jamii, kuongeza mishahara watumishi, kuongezea kwenye ujenzi wa SGR.

its_me_hery amesema kivp yaani...kwamba vyama vingine haviruhusiwi kushiriki huku relishaaaaaCjawahi kupiga kura na ctokuja kujichosha kupiga kura na kupoteza muda wangu kupanga folen bora nilale nyumban

Karagho Tusoke amesema nimeisikia kisha nikajisemea moyoni tunaipeleka wapi nchi yetu kisha wenyeww wanashangilia na kupiga makofi huku Tobiasi Paulo anahoji, “sasa kama ni kuwa ccm pekee uchaguzi wa nini.”

abeid_tz amesema tafsiri nyingine ni kwamba maamuzi kama hayo ni dalili za kuikandamiza na kuiondoa kabisa demokrasia nchini maana moja kati ya misingi ya demokrasia ni mfumo hai wa vyama vingi. Watoa hoja watuambie wanatumia kifungu kipi cha sheria na ibara gani ya katiba inahalalisha maamuzi kama hayo. Sijui aliye asisi haya maono anania ipi na Tanzania yetu.

Naye Rail Donald amesema, “dawa ni kuchagua wabunge wengi wa vyama vya upinzani hapo 2020 ila rais yeye tumuache aendelee tu ila wabunge wengi wawe wa vyama pinzani kama wafanyavyo mataifa mengine kama Marekani, Uingereza na kwingineko na hii itakomesha zile ndiooo na kuleta haki katika maamuzi ya mambo yahusuyo wananch na mali zao.”