InDriver yatua Arusha, abiria kuchipangia bei

Tuesday November 13 2018

By Ephrahim Bahemu, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Kampuni ya kimataifa ya usafiri kimtandao ya inDriver imeingia barani Afrika kwa kuanzia katika jiji la utalii la Arusha nchini hapa.

InDriver ambayo makao yake makuu yapo New York nchini Marekani inafuata nyayo za Uber na Taxify ambazo zimekuwepo katika baadhi ya majiji lakini zote zilianzia jiji la biashara la Dar e s Salaam.

Tofauti na kampuni hizo zilizotangulia inDriver wasafiri ndiyo wanaojipangia bei  kulinga na mahali wanapokwenda, madereva wao huangalia na kuchagua nani ameweka bei nzuri inayofaa kwa safari husika.

Katika taarifa ya kampuni hiyo Mkurugenzi kitengo cha Biashara, inDriver Ygor Fedorov anasema kwa sasa hakuna makato wala malipo ya ziada kwa madereva wanaotoa huduma.

“Arusha ni mji wa kwanza Tanzania na barani Afrika ambapo Programu ya inDriver ilizinduliwa, huduma hii imeunganisha zaidi ya madereva 300 jijini Arusha na wengine wakizidi kusajiliwa kila siku,” amesema Fedorov.

Advertisement