Kutofuata uzazi wa mpango kwakwamisha ukuaji wa uchumi

Sunday June 16 2019

By Lilian Lucas, Mwananchi [email protected]

Morogoro. Meneja utetezi toka shirika la kimataifa la Uzazi wa Mpango (AFP) James Mlali, amesema endapo wanandoa watapanga idadi ya watoto wanaoweza kuwahudumia, kuna uhakika wa familia na Taifa kuendelea kukua kiuchumi.

Amesema jamii inatakiwa kuzingatia umuhimu wa afya ya uzazi wa mpango huku akieleza kuwa kwa mwaka 2018, asilimia 32 ya wanawake nchini wamekuwa wakitumia njia za kisasa za uzazi wa mpango.

Hivyo, ameitaka Serikali kuendelea kuweka nguvu ya kutosha ili kufikia azma ya asilimia 45 ifikapo mwaka 2020.

Mlali ambaye pia alikuwa mwezeshaji wa mafunzo ya Afya ya uzazi kwa Waandishi wa Habari za afya yaliyofadhiliwa na Taasisi ya Tanzania Communications Center (TCDC) chini ya mradi wa Advance Family Planning  AFP, amesema uzazi wa mpango ni muhimu ukapewa kipaumbele.

Mmoja wa  washiriki wa warsha hiyo,  James Range akichangia  mada amesema kukiwa na watoa huduma wenye sifa, elimu ya uzazi wa mpango itawafikia walengwa wote na kutoa nafasi kwa mhitaji kuchagua atumie njia gani.

Advertisement