Leo mwisho wa kampeni Nigeria

Thursday February 14 2019

Lagos, Nigeria. Leo ni siku ya mwisho ya kampeni za uchaguzi mkuu nchini Nigeria ambao utafanyika Jumamosi.

Nigeria ilifanikiwa kuingia katika uongozi wa kidemokrasia miaka minne tu iliyopita licha ya matatizo mbalimbali wanayokumbana nayo hivi sasa.

Kampeni za uchaguzi zikisindikizwa na tungo za muziki kutoka kwa wasanii mbalimbali, Rais wa sasa ambaye anawania tena nafasi hiyo, Mohamud Buhari ameahidi kupeleka nchi hiyo katika hatua nyingine ya maendeleo endapo atachaguliwa.

Buhari ndiye alikua mwanasiasa wa kwanza wa upinzani kushinda uchaguzi wa nchi hiyo. Mapema wakati akifungua kampeni zake mwaka jana alisema: ‘’Vita ilianza muhula wa kwanza nahitaji kuendelea’’.

''Tunawajibika kuwa kazi tuliyoanza muhula wa kwanza ya kuhakikisha mali za nchi na rasilimali zinakua na umuhimu kwa wananchi wa kawaida'' alisema Buhari.

Hata hivyo, kuna maswali juu ya afya ya Buhari mwenye umri wa miaka 76 kwani amekua akisafiri mara kwa mara kwenda London Uingereza kwa matibabu ya ugonjwa ambao umewekwa siri.


Advertisement