Macho na masikio bungeni Dodoma

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango akiwasilisha bungeni hali ya uchumi wa taifa kwa mwaka wa fedha 2018 na mpango wa maendeleo wa taifa wa mwaka wa fedha 2019/2020, jijini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi

Muktasari:

Bajeti kuu ya Serikali mwaka 2019/2020 itawasilishwa bungeni jijini Dodoma leo Alhamisi Juni 13, 2019 saa 10 jioni na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango. Kabla ya kuwasilishwa kwa bajeti hiyo leo asubuhi, Dk Mpango atawasilisha taarifa ya hali ya uchumi wa Taifa mwaka 2018 na Mpango wa Maendeleo wa  Taifa mwaka 2019/2020.

Dodoma. Ni kawaida kusikia sauti ya Rais John Magufuli redioni kila mara ikiwasisitizia wananchi kudai risiti kwa kila bidhaa wanayonunua ili Serikali ya Tanzania ipate kodi yake ya kuwezesha kutoa huduma kwa wananchi.

Kauli hiyo ndiyo inategemea kuakisiwa kwenye maeneo mengi ya Hotuba ya Makadirio na Matumizi ya Serikali kwa mwaka 2019/2020 itakayosomwa leo Alhamisi Juni 13, 2019 na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Phillip Mpango bungeni mjini Dodoma.

Kwa mujibu wa hotuba ya kiwango na ukomo wa bajeti ya mwaka 2019/2020 iliyowasilishwa Machi, 2019 na Dk Mpango, serikali inatarajia kukusanya na kutumia Sh33.1 trilioni.

Serikali kuu itakusanya Sh22.2 trilioni, kati ya hayo yanayotokana na kodi (TRA) ni Sh 19.1 trilioni na mapato yasiyo ya kodi ni Sh 3.1trilioni, na mapato yanayotokana na halmashauri katika mwaka huu yatakuwa ni Sh 765.4bilioni.

Waziri huyo alisema mikopo ya ndani na nje itakuwa Sh 7.27 trilioni ambapo kati ya hiyo Sh 4.96 trilioni ni mikopo ya ndani na mikopo ya nje yenye masharti ya kibiashara inakadiriwa kuwa Sh 2.31trilioni.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi kuhusu bajeti mwaka 2019/2020