VIDEO: Magufuli awataka wafanyabiashara kuzieleza changamoto zao

Muktasari:

Leo Ijumaa, Rais wa Tanzania, John Magufuli amekutana na wafanyabiashara kutoka wilaya zote nchini Ikulu jijini Dar es Salaam na kuwataka kuwa wazi kueleza changamoto zinazowakabili ili ziweze kutafutiwa ufumbuzi 

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Magufuli amekutana na wawakilishi wa wafanyabiashara kutoka wilaya zote nchini na kuwataka wawe wazi kueleza changamoto zilizopo ili zipatiwe ufumbuzi.

Rais Magufuli amesema hayo leo Ijumaa Juni 7, 2019 Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo ameanza kwa kuelezea mafanikio mbalimbali ya Serikali  anayoiongoza tangu iingie madarakani Novemba 5 mwaka 2015.

Amesema kikoa hicho kitasaidia kuboresha mazingira ya biashara na kwa kuona umuhimu wa kikao hicho, amewalika mawaziri na wakuu wa vyombo vya dola  kusikiliza yale yatakayosemwa na wafanyabiashara na hatua zianze kuchukuliwa.

Magufuli amesema kuzungumza na wafanyabiashara wa aina mbalimbali itawasaidia kuwa na lengo la aina moja na kuwataka kuzungumza ukweli ili kupata suluhisho.

“Sekta ya biashara ni muhimu kwa maendeleo ya nchini ndiyo maana Serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali za kuboresha mazingira ya biashara nchini na kuimarisha amani na usalama,” amesema Magufuli

“Kwenye amani ndipo biashara hufanyika, kinyume chake kila kitu kinakuwa tofauti ndiyo maana tumekuwa tukijitahidi sana kulinda amani kwa kujitahidi kuzuia vitendo vya unyang’anyi, uporaji kwa kutumia silaha,” amesema.

Amesema kupambana na vitendo vya rushwa pia ni njia moja wapo wa kuchochea ukuaji wa kibiashara, kuboresha upatikanaji wa umeme, kuboresha miundombinu.

 

Endelea kufuatilia Mwananchi