Magufuli amtumbua Makala, ampeleka Homera Katavi

Muktasari:

  • Rais Magufuli ametengua uteuzi wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Amos Makalla na nafasi yake kumpangia Juma Homera aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Tunduru.

Dar es Salaam. Rais John Magufuli amempandisha hadhi aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Juma Homera kuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi kuanzia leo, Mei 14,2019.
Uteuzi huo wa Homera umetokana na uamuzi wa wa Rais kumpumzisha aliyekuwa mkuu wa mkoa huo, Amos Makala.
Taarifa iliyotolewa na mkurugenzi wa kurugenzi ya mawasiliano ikulu, Gerson Msigwa inasema “uteuzi wa mkuu wa Wilaya ya Tunduru utafanywa baadaye.”
Homera aliteuliwa kuiongoza Wilaya ya Tunduru mwaka 2016 na mpaka anapandishwa wadhfa huu, alikuwa hajahamishwa eneo hilo la kazi.
“Namshukuru mheshimiwa Rais kwa kuniamini ila amenipa majukumu mazito. Nitajifunza na kumsaidia kadri ya uwezo wangu,” amesema Homera alipozungumza na Mwananchi kw anjia ya simu.
Kabla ya kupelekwa Katavi Julai mwaka jana, Makalla alikuwa mkuu wa Mkoa wa Mbeya alikodumu tangu mwaka 2016 Dk Magufuli alipofanya uteuzi wa kwanza wa wakuu wa mikoa na wilaya.