Majaliwa, Ndugai awataka Watanzania kuombea amani

Wednesday May 15 2019

By Habel Chidawali, Mwananchi [email protected]

Dodoma. Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa amewaomba Watanzania kuungana na Waislamu wote nchini katika kipindi hiki cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan kuliombea taifa.

Majaliwa ametoa rai hiyo Jumatano Mei 15 wakati akiwakaribisha wabunge na watumishi kwenye futari aliyowaandalia nyumbani kwake mjini Dodoma.

Amesema katika kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani Waislamu wanaendelea kuombea amani hivyo na watu wengine waungane nao.

Kauli hiyo ya Majaliwa iliungwa mkono na Spika, Job Ndugai akisema kipindi cha mfungo wa Ramadhan ni muhumi kuombea amani.

Spika amewataka wasiofunga waendelee kufuatilia mawaidha mbalimbali yanayotolewa na viongozi wa dini hiyo.

Kwa upande wake, kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, Joseph Selasini amesema ni jambo jema ndugu wakikaa pamoja na kumpongeza waziri mkuu kwa kufanya jambo jema.

Advertisement

 

Advertisement