Majaliwa ataka watendaji kutokaa ofisini

Waziri Mkuu wa Tanzania,  Kassim Majaliwa

Muktasari:

  • Waziri Mkuu wa Tanzania,  Kassim Majaliwa amewataka viongozi na watendaji kutokaa ofisini, kuwataka kwenda vijijini kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi

Same. Waziri Mkuu wa Tanzania,  Kassim Majaliwa amewataka viongozi na watendaji kutokaa ofisini, kuwataka kwenda vijijini kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi.

Ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Julai 19, 2019 wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri ya Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro.

Amesema kila mtumishi lazima atambue jukumu  lake la kuwatumikia wananchi na Serikali haitarajii kusikia malalamiko ya wananchi kuhusu watendaji kutowajibika.

"Watumishi wa umma msikae ofisini nendeni vijijini mkashughulike na matatizo ya wananchi, tumewapa magari, nendeni vijijini mkawatumikie wananchi kwa sababu hawana nauli za kuwafuata ofisini kuleta matatizo yao," amesema Majaliwa.

Amemtaka mkuu wa Wilaya na katibu tawala wa Wilaya ya Same kuwasimamia watendaji na kuhakikisha wanasikiliza  kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi.

Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Senyamule  amesema Serikali imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.