VIDEO: Makamba: Kikwete alinivutia kuingia katika siasa

Muktasari:

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba amemtaja Rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete kuwa ndio aliyemvutia kuingia katika siasa


Dar es Salaam. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba amemtaja Rais mstaafu wa Tanzania, Jakaya Kikwete kuwa ndio aliyemvutia kuingia katika siasa.

January ambaye ni mbunge wa Bumbuli (CCM) amesema baba yake, Yusuf Makamba aliyewahi kuwa mkuu wa Mkoa na katibu mkuu wa CCM, si aliyemvutia kuingia katika siasa.

Akizungumza na Mwananchi, Makamba amesema rais huyo mstaafu wa Awamu ya Nne alimvutia kwa sababu alimpa nafasi ya kufanya kazi pamoja kwenye ulingo wa siasa.

Kuhusu baba yake, Makamba amesema hakuwahi kumvutia kwenye siasa kwa sababu ni mzee wake na kuna wakati alimuogopa hadi kumkimbia.

January Makamba alianza kufanya kazi na Kikwete alipokuwa akifanya mafunzo kwa vitendo katika Wizara ya Mambo ya Nje mwaka 2005 hadi 2010.