Makinikia yaibukia hotuba ya Waziri Mkuu

Mbunge wa Kuteuliwa, Abdallah Bulembo akichangia bungeni mjadala wa kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2019/2020, jijini Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuz

Dodoma. Sakata kuhusu mchanga wa makinikia, ubaguzi wa kiitikadi na kufungwa kwa maduka ya fedha jana yaliibuka bungeni wakati wa mjadala hotuba ya bajeti ya Ofisi ya waziri Mkuu, wakati wabunge walipotaka masuala hayo yaangaliwe upya.

Serikali ilipiga marufuku kusafirishwa kwenda nje kwa mchanga huo Machi 3, 2017 na kusababisha mgogoro baina yake na kampuni ya Acacia. Acacia ilikuwa inasafirisha mchanga huo kwa ajili ya kwenda kuuyeyusha kupata masalia ya madini baada ya dhahabu kupatikana katika hatua ya kwanza ya uchenjuaji mgodini.

Mbali na kuiathiri kampuni hiyo, zuio la kusafirisha makinikia nje pia liliathiri wachimbaji wadogo ambao waliiangukia Serikali wakisema wanaingia gharama kubwa za kutunza makontena yenye mchanga huo na kusimamisha uchimbaji.

Pia Serikali imedhibiti maduka ya kubadilishia fedha na kusababisha mengi kufungwa, huku kukiwa na taarifa kuwa itapeleka muswada bungeni kudhibiti zaidi.

Jana, mbunge wa kuteuliwa na Rais, Abdallah Bulembo aliishauri Serikali kuruhusu watu kusafirisha mchanga huo badala ya kuendelea kuwazuia.

Bulembo alisema kuwazuia kusafirisha nje kunasababisha Serikali ikose mapato na pia kuathiri wachimbaji ambao hawana madoa.

“Kuna wenzetu hawana matatizo ya kulipa kodi na wako tayari kulipa kodi kwa nini hamuwapi ruhusa Serikali ikapata pesa yake, wanakosa gani hawa?” alihoji Bulembo.

“Naomba kosa la mtoto mmoja lisimzuie mtoto mwingine kupata haki yake ya maisha. Nakuombeni sana watu wa madini nendeni mkaangalie eneo hili.”

Kwa mujibu wa Acacia, ndani ya makinikia dhahabu ni asilimia 90, shaba na fedha asilimia 10 ya thamani.

Serikali inasema kuwa Acacia ilikuwa inadanganya kuhusu kiwango cha dhahabu na shaba kilichomo kwenye makinikia na kutaka uyeyushaji ufanyike ndani ya nchi.

Machi 29, wachimbaji wadogo walikutana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam na kutoa kilio chao kwa Serikali wakitaka waruhusiwe kuendelea kusafirisha nje. Hadi sasa , kitu alichosema kinaikosesha Serikali mapato na kuwazuia.

Wakati Bulembo akiibuka na makinikia, mbunge wa Baraza la Wawakilishi (BLW), Jaku Hashim Ayub aliitaka Serikali kuweka masharti yenye uwiano katika biashara ya maduka ya kubadilisha fedha za kigeni.

Jaku ametoa kauli hiyo ikiwa zimepita siku tani tangu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango kusema Serikali imeandaa kanuni mpya kwa ajili ya biashara hiyo ya fedha ambazo zitaelekeza jinsi ya kuomba leseni za uendeshaji wa maduka.

Alisema kwa kuzingatia maduka mengi yaliyokaguliwa yamefungwa, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imechukua tahadhari kuhakikisha huduma ya ubadilishaji fedha za kigeni inaendelea.

Lakini jana, Jaku alisema mambo mengi Tanzania Bara imeiga kutoka Zanzibar na kwamba amesikia kuwa kanuni ya maduka itakuwa ngumu.

“Zanzibar ni ndogo inategemea sana utalii na muangalie masharti yaliyopo yawe na uwiano. Zanzibar inategemea utalii na watalii watapata shida. Fomula itasokota sana wananchi,” alisema.

nchini kwa kutolewa na benki zote pamoja na Shirika la Posta.

Demokrasia

Naye mbunge Moshi Mjini (Chadema), Jaffary Michael alizungumzia suala la demokrasia akibainisha kuwa imekuwa mbaya zaidi katika utawala wa sasa.

“Katika nchi hii hakuna ubaguzi wa kidini wala kikabila, lakini kuna ubaguzi wa kiitikadi. Wapo watu wanaoona mtu mwenye itikadi tofauti na CCM hana haki ya kuishi,” alisema.