Mama Abdul wa Mambo Hayo afariki dunia

Friday January 25 2019
mamaabdulipic

Salome Nonge maaurufu kwa jina la ‘Mama Abdul’

Dar es Salaam. Muigizaji wa siku nyingi Salome Nonge maaurufu ‘Mama Abduli’ amefariki dunia.

Mama Abdul ambaye alipata umaarufu kupitia kundi la Nyota Ensemble lililotesa na michezo mbalimbali ikiwemo 'Mambo Hayo'.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa leo Januari 25, 2019 na Ofisa Habari wa Chama cha Waigizaji Kinondoni (TDFAA) Masoud Kaftany.

Katika taarifa hiyo, ilisema kuwa mama Abdul amefariki leo mchana nyumbani kwake maeneo ya Mburahati.

Kwa mujibu wa Kaftany msiba upo nyumbani kwake na  taratibu za mazishi zitatolewa  baada ya kikao.

Kabla ya mauti mama Abdul alikuwa akionekana katika kipindi cha vichekesho cha Mwantumu kinachorushwa chaneli ya Maisha Magic Bongo katika king’amuzi cha DsTV.

Advertisement

Humo ndani amecheza na wasanii mbalimbali akiwemo Baba James na Joti.


Advertisement